Waliimba kwa kupokezana, wakimsifu na kumtukuza Mwenyezi-Mungu:“Kwa kuwa yu mwema,fadhili zake kwa Israeli zadumu milele.”Watu wote walipaza sauti kwa nguvu zao zote, wakamsifu Mwenyezi-Mungu kwa sababu ya kuanza kujengwa msingi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu.