Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 34:16-29 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,

17. “Kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni ndio watakaowagawia watu nchi kuwa mali yao.

18. Utachukua pia kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia katika ugawaji wa nchi.

19. Haya ndiyo majina yao:Kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.

20. Kabila la Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.

21. Kabila la Benyamini, Elidadi mwana wa Kisloni.

22. Kabila la Dani, Buki mwana wa Yogli.

23. Kabila la Manase mwanawe Yosefu, Hanieli mwana wa Efodi.

24. Kabila la Efraimu, mwanawe Yosefu, Kemueli mwana wa Shiftani.

25. Kabila la Zebuluni, Elisafani mwana wa Parnaki.

26. Kabila la Isakari, Paltieli mwana wa Azani.

27. Kabila la Asheri, Ahihudi mwana wa Shelomi

28. Kabila la Naftali, Pedaheli mwana wa Amihudi.

29. Hawa ndio watu ambao Mwenyezi-Mungu aliwaamuru wawagawie Waisraeli nchi ya Kanaani kuwa mali yao.”

Kusoma sura kamili Hesabu 34