Agano la Kale

Agano Jipya

Kumbukumbu La Sheria 32:18-31 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Hamkumjali Mwamba aliyewapa uhai,mlimsahau Mungu aliyewazaa nyinyi.

19. Mwenyezi-Mungu aliona jambo hilo akawaacha;aliwakataa watoto wake, waume kwa wake.

20. Akasema, ‘Nitawaficha uso wangunione mwisho wao utakuwaje!Maana wao ni kizazi kipotovu,watoto wasio na uaminifu wowote.

21. Wamenichochea kuona wivu kwa kitu kisicho mungu,wamenikasirisha kwa sanamu zao.Hivyo nitawafanya waone wivu kwa kisicho watu,nitawakasirisha kwa kutumia taifa la wapumbavu.

22. Hasira yangu imewaka moto,inachoma mpaka chini kuzimu,itateketeza dunia na vilivyomo,itaunguza misingi ya milima.

23. Nitarundika maafa chungu nzima juu yao,nitawamalizia mishale yangu.

24. Watakonda kwa njaa,wataangamizwa kwa homa kali.Nitapeleka wanyama wenye meno makali kuwashambulia,na nyoka wenye sumu wanaotambaa mavumbini.

25. Vita vitasababisha vifo vingi njena majumbani hofu itawatawala,vijana wa kiume na wa kike watauawahata wanyonyao na wazee wenye mvi.

26. Nilisema, ningaliwaangamiza kabisana kuwafanya wasikumbukwe tena na mtu yeyote,

27. ila tu kwa sababu ya majivuno ya maadui zaoili maadui zao wasije wakafikiria vingine;wasije wakasema, wamefaulu kuwaangamiza,nami Mwenyezi-Mungu sihusiki katika mambo haya!’

28. “Israeli ni taifa lisilo na akili,watu wake hawana busara ndani yao.

29. Wangekuwa na hekima wangejua kwa nini walishindwa,wangeweza kuelewa mwisho wao utakuwaje.

30. Mtu mmoja anawezaje kuwashinda watu 1,000,au watu wawili wanawezaje kuwashinda watu 10,000,isipokuwa kama Mwamba wao amewatupa,Mwenyezi-Mungu wao amewaacha?

31. Hata adui zetu wenyewe wamekiri wazi,mwamba wao hauna nguvu kama mwamba wetu.

Kusoma sura kamili Kumbukumbu La Sheria 32