Agano la Kale

Agano Jipya

Walawi 6:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,

2. “Ikiwa mtu yeyote ametenda dhambi na kumwasi Mwenyezi-Mungu kwa kumdanganya jirani yake juu ya amana au dhamana aliyowekewa, au kumnyanganya au amemdhulumu mwenzake,

3. au amepata kitu cha jirani yake kilichopotea, akasema kwamba hakukiona, au ameapa uongo juu ya chochote ambacho watu hufanya wakawa na hatia,

4. mtu huyo anapokuwa ametenda dhambi na amekuwa na hatia, ni lazima arudishe alichoiba au alichopata kwa dhuluma, au amana aliyopewa, au kitu cha jirani yake kilichopotea akakipata,

5. au chochote alichoapa kwa uongo. Atalipa kila kitu kikamilifu na kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Mara atakapojua kosa lake atamrudishia mwenyewe.

6. Kisha atamletea kuhani kondoo dume au mbuzi dume asiye na dosari amtolee Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa hatia; thamani ya mnyama huyo itakuwa ile ya kawaida ya kuondoa hatia.

7. Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu, naye atasamehewa kosa ambalo alikuwa amelifanya.”

8. Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,

9. “Mpe Aroni na wanawe maagizo haya: Ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuteketezwa. Sadaka ya kuteketezwa itakuwa motoni juu ya madhabahu usiku kucha hadi asubuhi na moto wake uchochewe, usizimike.

10. Kisha kuhani akiwa amevaa vazi lake rasmi la kitani na kaptura yake ya kitani, atachukua majivu ya ile sadaka kutoka madhabahuni na kuyaweka kando ya madhabahu.

11. Halafu baada ya kubadilisha mavazi yake atayapeleka yale majivu nje ya kambi mahali palipo safi.

Kusoma sura kamili Walawi 6