Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29

Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 20 Biblia Habari Njema (BHN)

Daudi anauteka mji wa Raba

1. Hata ikawa katika mwanzo wa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi na kuteka nyara nchi ya Waamoni, pia akaenda na kuuzingira Raba. Lakini Daudi alibaki huko Yerusalemu. Naye Yoabu aliushambulia Raba na kuuharibu;

2. naye Daudi akaichukua taji ya mungu wao Milkomu kichwani pake; naye aligundua ya kwamba taji hiyo ilikuwa na uzito wa kilo thelathini na tano za dhahabu na ndani yake mlikuwemo kito cha thamani. Naye Daudi akakitwaa kupambia taji yake. Pia, aliteka idadi kubwa ya nyara kutoka katika mji huo.

3. Halafu aliwachukua watu wa mji huo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sururu za chuma na mashoka ya chuma. Hivyo ndivyo alivyoitenda miji yote ya Waamoni. Hatimaye Daudi na watu wote wakarudi Yerusalemu.

Vita na majitu ya Wafilisti

4. Baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gezeri. Sibekai, Mhushathi, akamuua Sipai aliyekuwa mmojawapo wa wazawa wa Warefai; hivyo Wafilisti wakawa wameshindwa.

5. Kulitokea tena vita na Wafilisti. Naye Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake, ulikuwa kama mti wa mfumaji.

6. Baadaye kulitokea tena vita huko Gathi ambako kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na kimo kikubwa, na vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu, jumla yake vidole ishirini na vinne. Yeye pia alikuwa mzawa wa majitu.

7. Naye alipowatukana Waisraeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, alimuua.

8. Hao walikuwa wazawa wa majitu huko Gathi; nao waliuawa na Daudi pamoja na watumishi wake.