Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 1:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa pili, mwaka wa pili baada ya wana wa Israeli kutoka Misri, Mwenyezi-Mungu aliongea na Mose ndani ya hema la mkutano jangwani Sinai, akamwambia hivi:

2. “Wewe na Aroni fanyeni sensa ya jumuiya yote ya Waisraeli, familia mojamoja kwa kufuata koo zao na idadi ya majina yao kila mwanamume mmojammoja;

3. wale wote katika Israeli wanaoweza kwenda vitani, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, mtawaweka katika orodha ya vikosi vikosi.

4. Tena mwanamume mmoja wa kila kabila atakuwa pamoja nanyi, kila mmoja aliye kiongozi wa jamaa za kabila lake.

5. Haya ndiyo majina ya watu watakaokusaidia:Kabila la Reubeni: Elisuri, mwana wa Shedeuri;

6. Kabila la Simeoni: Shelumieli mwana wa Suri-shadai;

Kusoma sura kamili Hesabu 1