Agano la Kale

Agano Jipya

Walawi 24:13-23 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,

14. “Mtoe kijana aliyekufuru nje ya kambi, na wale wote waliomsikia akikufuru waweke mikono yao juu ya kichwa chake, na jumuiya yote imuue kwa kumpiga mawe.

15. Nawe uwaambie Waisraeli kwamba mtu yeyote atakayemlaani Mungu wake ni lazima awajibike kwa dhambi yake.

16. Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni anayemkufuru Mwenyezi-Mungu, jumuiya nzima itamuua kwa kumpiga mawe.

17. Mtu yeyote anayeua mtu mwingine ni lazima naye auawe.

18. Mtu yeyote anayeua mnyama ni lazima atoe fidia: Uhai kwa uhai.

19. Mtu yeyote anayemwumiza jirani, ni lazima naye aumizwe kulingana na kiasi alichomwumiza jirani yake,

20. amemvunja mfupa naye atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kila mtu anayemwumiza mwenzake ni lazima naye aumizwe kulingana na tendo lake.

21. Anayemuua mnyama ni lazima atoe fidia; lakini mtu yeyote akimuua mtu mwingine ni lazima naye auawe.

22. Sheria hii yamhusu mgeni na mwenyeji. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”

23. Basi, Mose akawaambia Waisraeli hayo yote. Wakampeleka yule mtu aliyemlaani Mwenyezi-Mungu nje ya kambi, wakamuua kwa kumpiga mawe. Ndivyo Waisraeli walivyofanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Kusoma sura kamili Walawi 24