Agano la Kale

Agano Jipya

1 Wathesalonike 2:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ndugu, nyinyi wenyewe mnafahamu kwamba ziara yetu kwenu haikuwa bure.

2. Mnajua jinsi tulivyodhulumiwa na kutukanwa kule Filipi kabla ya kufika kwenu Thesalonike. Ingawa kulikuwa na upinzani mwingi, Mungu wetu alitujalia uhodari wa kuwahubirieni Habari Njema yake.

3. Jambo tunalosisitiza kwenu si jambo linalotegemea uongo au nia mbaya; wala hatupendi kumdanganya mtu yeyote.

4. Sisi twanena daima kama atakavyo Mungu kwani yeye alituona kwamba tunafaa, akatukabidhi hii Habari Njema. Si nia yetu kuwapendeza watu hata kidogo, bali twataka kumpendeza Mungu ambaye anajua mioyo yetu mpaka ndani.

5. Maana kama mjuavyo, sisi hatukutumia maneno ya kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi fulani; Mungu ni shahidi!

6. Hatukutafuta sifa kutoka kwa watu, wala kutoka kwenu, wala kutoka kwa mtu yeyote,

7. ingawa sisi tukiwa mitume wa Kristo, tungeweza kudai mambo fulani kwenu. Lakini sisi tulikuwa wapole kati yenu kama alivyo mama kwa watoto wake.

Kusoma sura kamili 1 Wathesalonike 2