Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42
  43. 43
  44. 44
  45. 45
  46. 46
  47. 47
  48. 48
  49. 49
  50. 50
  51. 51
  52. 52
  53. 53
  54. 54
  55. 55
  56. 56
  57. 57
  58. 58
  59. 59
  60. 60
  61. 61
  62. 62
  63. 63
  64. 64
  65. 65
  66. 66

Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 32 Biblia Habari Njema (BHN)

Mfalme mwadilifu

1. Kutatokea mfalme atakayetawala kwa uadilifu,nao viongozi wataongoza kwa kufuata haki.

2. Kila mmoja atakuwa kama mahali pa kujikinga na upepo,kama mahali pa kujificha wakati wa tufani.Watakuwa kama vijito vya maji katika nchi kame,kama kivuli cha mwamba mkubwa jangwani.

3. Macho hayatafumbwa tena,masikio yatabaki wazi.

4. Wafanyao mambo kwa hamaki wataamua kwa busara,wenye kigugumizi wataongea sawasawa.

5. Wapumbavu hawataitwa tena waungwana,wala walaghai hawataitwa tena waheshimiwa.

6. Wapumbavu hunena upumbavu,na fikira zao hupanga kutenda uovu,kutenda mambo yasiyo mema,kusema mambo ya kumkufuru Mwenyezi-Mungu.Huwaacha wenye njaa bila chakula,na wenye kiu huwanyima kinywaji.

7. Ulaghai wa walaghai ni mbaya;hao huzua visa viovu,na kumwangamiza maskini kwa maneno ya uongo,hata kama madai ya maskini ni halali.

8. Lakini waungwana hutenda kiungwana,nao hutetea mambo ya kiungwana.

Mawaidha kwa wanawake wa Yerusalemu

9. Inukeni, enyi wanawake mnaostarehe, mnisikilize;sikilizeni ninayosema enyi mabinti mlioridhika.

10. Katika mwaka mmoja hivi mtatetemeka nyinyi mliotosheka;maana hamtapata mavuno yoyote,na mavuno ya zabibu yatatoweka.

11. Tetemekeni kwa woga, enyi mnaojikalia tu;tetemekeni kwa hofu, enyi mnaostarehe!Vueni nguo zenu, mbaki uchi,mjifunge vazi la gunia viunoni mwenu.

12. Jipigeni vifua kwa huzuni,ombolezeni, kwa sababu ya bustani zilizokuwa nzuri,kwa mizabibu iliyokuwa ikizaa sana,

13. kwa ardhi ya watu wangu inayoota miiba na mbigili,kwa nyumba zote zilizojaa watu wenye furaha,kwa mji uliokuwa na shangwe.

14. Maana ikulu ya mfalme itaachwa mahame,mji huo wa watu wengi utahamwa.Mlima na mnara wa ulinzi utakuwa mapango milele,pundamwitu watapitapita huko kwa furaha,kondoo watapata malisho yao humo.

Nyakati za amani

15. Hali itaendelea kuwa hivyompaka tumiminiwe roho ya Mungu kutoka juu.Hapo jangwa litakuwa shamba la rutuba tena,na mashamba ya rutuba yatakuwa msitu.

16. Haki itadumu katika nchi iliyokuwa nyika,uadilifu utatawala katika mashamba yenye rutuba.

17. Kutokana na uadilifu watu watapata amani,utulivu na usalama utadumu milele.

18. Watu wangu watakaa katika makao ya amani,katika maskani salama na mazingira matulivu.

19. Msitu wa adui utatoweka kabisa,na mji wake utaangamizwa.

20. Lakini heri yenu nyinyi:Mtapanda mbegu zenu popote penye maji,ng'ombe na punda wenu watatembeatembea watakavyo.